Psalms 138

Maombi Ya Shukrani

(Zaburi Ya Daudi)


1 aNitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote,
mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako.

2 bNitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu,
nami nitalisifu jina lako
kwa ajili ya upendo wako
na uaminifu,
kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako
juu ya vitu vyote.

3 cNilipoita, ulinijibu;
ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.


4 dWafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana,
wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako.

5 eWao na waimbe kuhusu njia za Bwana,
kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.


6 fIngawa Bwana yuko juu,
humwangalia mnyonge,
bali mwenye kiburi
yeye anamjua kutokea mbali.

7 gNijapopita katikati ya shida,
wewe unayahifadhi maisha yangu,
unanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu,
kwa mkono wako wa kuume unaniokoa.

8 h Bwana atatimiza kusudi lake kwangu,
Ee Bwana, upendo wako wadumu milele:
usiziache kazi za mikono yako.
Copyright information for SwhKC